Showing posts with label Yanga. Show all posts
Showing posts with label Yanga. Show all posts

Dili la Msuva Kutua Yanga Baba Yake Afunguka Ukweli

 

Kumekua na tetesi nyingi kuhusu Simon Msuva nyota wa zamani wa Yanga, Akihusishwa na kujiunga na Klabu ya Yanga Sc.

Taarifa zilizopo ni kwamba mzazi wa Msuva amesema tetesi za msuva kwenda yanga yeye anazo.

Mzazi huyo ambaye ni msimamizi wa staa huyo wa zamani wa Yanga, amekiri kusikia mwanae akihusishwa na Yanga  lakini amesema anachojua kwa sasa akili ya Msuva haipo Tanzania.

Bao la Kwanza la Yanga dhidi ya KMC Ilikua Faulo

 



"Ushindi wa jana wa Yanga 70% percent umetokana na makosa ya KMC, na Ubora wa Yanga ni kwa 30% percent"


"KMC walikuwa na poor defending, tazama Aziz Ki alikuwa hakabwi vya kutosha.. Magoli (2) ya kwanza yametokana na mabeki kushindwa kukaba vya kutosha"


"Halafu ile kona iliozaa bao la (1) ilioanzishwa na Aziz Ki ilikuwa faulo kabla haijatokea, lile halikustahili kuwa goli"


TAZAMA HAPA


©️ Geof Lea

Mchambuzi wa Efm radio


READ MORE| SOMA ZAIDI


Yanga Vs KMC - Highlights ya Magoli Yote

 


Dakika 45 za burudani zilimalizika katika dimba la Azam Complex, Chamazi, Wananchi wanaupiga mwingi mpaka unamwagika.


HT: Yanga SC 1-0 KMC FC

⚽ Job 17'


Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.


Dakika 90 zumemalizika Kwa Magoli 5-0


FT: Yanga SC 5 -0 KMC FC


TAZAMA MAGOLI YOTE HAPA


Ratiba Ya Mechi za Leo NBC Premier League - 23/08/2023

 


Yanga Vs KMC Live


๐— ๐—”๐—ง๐—–๐—›๐——๐—”๐—ฌ๐Ÿ”ฐ


๐Ÿ† NBC Premier League 

⚽️ Young Africans SC Vs KMC FC

๐Ÿ“† 23.08.2023

๐ŸŸ Azam Complex, Chamazi

๐Ÿ•– 1:00 Usiku 


Kuelekea Mechi Yetu v KMC Kwenye Head To Head Tangu Timu Ya KMC ilipopanda Daraja Na Kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara 


Wamekutana Mara       :10

Yanga Kashinda Mara  :7

KMC Kashinda Mara    :1

Wametoka Sare Mara   :2

Yanga Magoli Kufunga :13

KMC Magoli Kufunga    :5

>> SOMA ZAIDI | READ MORE...

๐ŸŸ️ ⚽ Leo Tazama mpira live kupitia Simu,

 Bonyeza Link Hapa | NI BURE

๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://bit.ly/Watch-Tazama-video-Hapa


©Sokalive 

Siri Ya Yanga na Bruno Ngomezi Yavuja

 


BRUNO Gomez, ni mingoni mwa wachezaji ambao wapenzi wa Yanga  walitamani kumuona kikosini mwao  msimu huu, chanzo changu ndani ya Singida  FG, kimefunguka kuwa pamoja na watu wa Yanga kumtamani Bruno,  lakini Mbrazil huyo hakubaliki na uongozi wa juu pamoja na makocha wao.


“Kuna viongozi wa juu kabisa Yanga hawamkubali Bruno. Wanasema bado anahitaji muda zaidi wa kukomaa  kumudu kucheza Yanga japo wanaukubali uwezo wake. Nadhani  hata makocha (wa Yanga), hawamkubali sana ndio maana hukuona nguvu ikiwekwa kumsajili,” 


Kocha wa Singida, Hans van der Pluijm  alipoulizwa iwapo kiungo huyo ana  nafasi katika kikosi cha Yanga, alisema:  “Bruno ni mchezaji mzuri, ila bado anahitaji kukua zaidi kuweza kuhimili kucheza Yanga. Kuchezea Yanga au  Simba si kitu kidogo, kule unahitaji uwe  umekomaa hasa kuweza kukabiliana na presha za mchezo na mashabiki. “Kule  Yanga anaweza kukosea mara moja,  mara mbili, mara tatu... mashabiki  wakamzomea na kumtoa kabisa  mchezoni, hivyo anatakiwa kubaki hapa  (Singida) ili aendelee kukomaa zaidi.

SOMA ZAIDI...

.

.

.

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao

 



๐Ÿšจ OFFICIAL & CONFIRMED:

Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao kutoka Asec kwa Mkataba wa mwaka mmoja.

Yao (26) ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ช anahesabika kuwa beki bora wa kulia pia na ubora wa kucheza kama winga mshambuliaji na kupiga krosi  za mabao.

MFAHAMU KOUASSI ATTOHOULA.

Jina kamili: KOUASSI ATTOHOULA YAO.

Watu wa nyumbani kwao wanapenda kumuita kwa jina la KOUASSI ATTOHOULA YAO.

Raia wa Ivory coast

....Alizaliwa Anyama,Ivory coast

mnamo Dec 20,1996 (Age 26)

Ana urefu wa 1.68m.

Wakala :VV Consulting.


⬛ Nafasi anayochezea ni beki wa kulia

.... Nafasi nyingine anayoweza kucheza ni beki wa kushoto/winga.


Alianza maisha ya soka kwenye akademi ya Mimosas na kuitumikia akademi hiyo kwenye vikosi vya U17 na U19.


✅Julai  1,2017 akasajiliwa na klabu ya  Williamsville ya nchini humo akitumikia kwa miaka miwili.

✅Akauzwa kwenda klabu ya O.Khouribga ya nchini Morocco Jan 16,2019 aliitumikia kwa miezi 6 kisha akatolewa kwa mkopo kwenda kwenye klabu ya  Kawkab Marrak mnamo Julai 17,2019.


✅ Mnamo Sep 15,2019 baada ya mkataba wa mkopo kuisha  alirejea kwenye klabu yake ya O.Khouribga.

Na mkataba wake ndani ya klabu hiyo uliisha miezi miwili baade.


✅๐ŸŸกNdipo akajiunga tena na klabu ya Asec Mimosas ya Wakubwa Nov 9,2020.


 MASHINDANO YA CAF KAMA MCHEZAJI

✅ Amecheza jumla ya mechi 35 ya mashindano haya ya CAF ngazi ya vilabu.

...CAFCL

Amecheza mechi 27, kati ya hizo ni mechi 5 tu alitokea benchi.

..... CAFCC

Amecheza mechi 8, kati ya hizo ni mechi 1 tu alitokea benchi.


Akiwa ligi ya Morocco alicheza mechi 9 na kufunga goli 1.


Aug 27 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 25,miezi 8 na siku 7 alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast chini ya kocha Jean Louis Gasset.

Mpaka sasa ameichezea hiyo ya taifa (michuano ya CHAN,na timu ya taifa ya pamoja) michezo 6.


Aliwahi kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu Ivory Coast 2021/22.

 Alikuwa miongoni kwa walioiunda kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Ivory Coast kwenye msimu wa 2021/22 na msimu uliopita wa 2022/23


 Mshindi wa Makombe mawili ya Ligi kuu Ivory Coast

 Mshindi wa  Makombe mawili ya FA.


Jezi Mpya Za Yanga Msimu Mpya Wa 2023/2024


Kama Ulikua hujaziona jezi mpya za Yanga SC hizi ndio zenyewe.



 Mbunifu wa jezi ya Nyeusi ya Yanga SC kwa msimu huu ameeleza maana ya jezi hiyo huku akijikita kwenye Michoro iliyopo, ameeleza kua;

Jezi ya nyeusi, ukiangalia inamichoro ya 88 na michoro hiyo ilivyokaa imekaa katika mafungu manne ambayo yanamadisha medali nne walizopata Klabu ya Yanga SC


Pia Ameeleza kua ndani ya michoro hiyo kuna Nyota, ambazo zinaeleza kizazi cha nyota au dhahabu ambacho ni Yannga SC ambayo imepitia wakati mzuri mzimu huu.


Kwa Chini kuna nyuzi mzunguko na nembo ambayo ina "Y"; huo mzunguko ulijishikiza katika nembo inawakilisha medali Yanga SC ilizopata na Hiyo Y inamanisha Yanga SC


Je, una maoni gani?

Mbunifu wa jezi ya Yanga SC kwa msimu huu ameeleza maana ya jezi ya njano huku akijikita kwenye Michoro iliyopo, ameeleza kua;

Jezi ya njano maana yake inaelezea matokeo mazuri ya kutokufungwa kwa klabu ya yanga mara nyingi na kutwaa ubigwa


Lakini pia ameeleza kuwa, ukiangalia michoro iliyopo ni ya mchezo mahili wa kupanga matofali ili yasoporomoke, mchezo ambo unahitaji akili na na weredi wa hali ya juu. 


Hiyo inamanisha mipango mathubuti iliyofanywa na Aliyekua kocha wa Yanga SC Nasreddine Nabi ya kuweka vizuri timu hiyo na kuvunja rekodi ya kutwaa ubingwa kwa msimu uliopita




Hizo ndizo jezi za Yanga Msimu huu wa 2023/2024

Breaking: Ukweli Kuhusu Mayele Na Yanga SC

 


Fahamu ukweli kuhusu mayele kuondoka Yanga Sc


Mayele mwenye mkataba wa mwaka mmoja na Yanga amegoma kusaini mkataba mpya ambao ungemfanya awe analipwa pesa ndefu kuliko mchezaji yeyote ndani ya timu hiyo huku akidaiwa amepagawa na ofa nono kutoka Esperance ya Tunisia, Zamalek, Pyramids za Misri,  timu za ubelgiji na Qatar.


Kikao hicho kilihusisha pia wasimamizi wa mchezaji huyo ambao wanapushi staa huyo akiwashe Arabuni ambako kuna mkwanja mnene na wako tayari kununua mkataba uliosalia Yanga



Bado hawajafikia muafaka wa kusalia au kuondoka ingawa tajiri ahidi dau nono lakini juzi mchana alionekana kwenye sehemu Jijini Dar es Salaam akipiga picha za matangazo ya uzi mpya wa Jangwani ambao umetangazwa jana usiku nchini Malawai.


Mshambuliaji huyo kupiga picha na uzi wa Yanga kwa ajili ya tangazo ni jambo ambalo linaashiria lolote linaweza kutokea.


Credit: Mwanaspoti

TANZIA: MWANA YANGA WAFARIKI

 

Yanga Wametoa Taarifa ya Shabiki aliyefariki katika ajali.



Wana Yanga Sc Wapata Ajali Leo

 



Taarifa Kutoka klabu ya Yanga Inasema,

"Kuna taarifa za Ajali maeneo ya Msata kwa Mashabiki wetu waliokuwa wakisafiri kuja Arusha kutazama mechi ya kesho. 


Tunaendelea kufuatilia kwa karibu, tutatoa taarifa rasmi. Kwasasa tunaomba Dua na Sala zenu๐Ÿ™๐Ÿฝ


#TimuYaWananchi..."

Machi Ya Coastal Union ๐Ÿ†š Young Africans SC

 ๐—ก๐—˜๐—ซ๐—ง ๐— ๐—”๐—ง๐—–๐—›๐Ÿ”ฐ



⚽️Coastal Union ๐Ÿ†š Young Africans SC

๐Ÿ—“ 20 Agosti 2022

⏱ 10:00 Jioni 

๐ŸŸ Uwanja wa Sheikh Amri Abeid 

๐Ÿ† #LigiKuu  


#TimuYaWananchi 

#DaimaMbeleNyumaMwiko 

Full Time: Yanga Sc Vs Polisi Tanzaniq



Clabu ya Yanga imeifunga timu ya Polisi Tanzania Ambapo Yanga Imeifunga Magoli Mawili Huku Polisi Tanzania Wakifunga Goli moja

 Mchezo umefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid


POLISI TZ 1-2 YANGA

⚽Kipemba 34'

⚽Mayele 42'

⚽Mwamnyeto 85'


Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara,Yanga wameanza kampeni za kuutetea ubingwa wao kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika dimba la Sheikh Amri Abeid 

YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL

YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL


Klabu ya Yanga imefikia makubaliano na klabu ya Singida Big Stars juu ya kubadilishana wachezaji Mbrazil Dario Federico Da'Silva JR na Jesus Moloko.


Mbrazil huyo atajiunga na Yanga SC huku Moloko akienda upande wa pili 


Kila kitu kinaenda sawa mezani huku dili hilo likitarajiwa kukamilika kabla ya dirisha kufungwa Agosti 31.


#KitengeSports

MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"

 

MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"


Aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema ameshiriki kwenye Siku ya Mwananchi kama mshereheshaji (MC) na sio kama mhamasishaji.

Manara amesema hayo baada ya kutambulisha kikosi cha Yanga mwaka 2022/2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

FULL TIME: YANGA SC 0-2 VIPERS FC



FULL TIME: YANGA SC 0-2 VIPERS FC


๐ŸŸ️ Benjamin Mkapa


YANGA SC 0-2 VIPERS FC

⚽ Karisa 1'

⚽ Anukani 65'


Shughuli imemalizika katika dimba la Benjamin Mkapa, Vipers wameharibu siku ya MWANANCHI baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji wao Yanga SC.


Magoli ya wageni yamefungwa na Milton Karisa na Bright Anukani.


Moriso Ashtukiwa, Apewa Siku 14

 

BERNARD Morrison ameanza kazi rasmi Yanga na leo akiingia siku ya nne mazoezini, lakini kocha mmoja fundi wa mazoezi ameshtukia kitu kwa winga huyo Mghana kisha akamtengea siku 14 za kazi nzito.

Kocha aliyemshtukia BM33 ni Helmy Gueldich ambaye ni kocha wa mazoezi ya viungo aliyeangalia ubora wa mshambuliaji huyo kisha akagundua kwamba jamaa hakufuata sawasawa ratiba ya mazoezi waliyomtumia.

Helmy hata hivyo ameliambia Mwanaspoti kwamba Morrison yuko nusu fiti - nusu unga, lakini ndani ya wiki mbili tu atakuwa katika daraja lingine la ubora.

Kocha huyo alisema katika ratiba ya wiki ya kwanza Morrison atakuwa na kazi ngumu ambayo itamsaidia baadaye kurudisha ubora.

“Tulimpatia ratiba mapema kabla ya kujiunga alitakiwa kuifanya kwa ukamilifu lakini nimemuangalia naona hakuifuata sawasawa ila atakuwa sawa,” alisema Helmy ambaye bado anahitajika Chama cha Soka Tunisia.

“Ni mchezaji mzuri (Morrison) sio mbaya kwa hali aliyokuja nayo kitu kibaya angekuwa hajafuata kabisa lakini tuna muda wa kumrudisha katika mstari.”

Juzi Morrison alikimbizwa mazoezini Yanga akizunguka peke yake pembeni kisha akasimama na kulalamika akiongea kwa Kiswahili akisema: “Huyu jamaa anaiua huyu’ kauli ambayo mashabiki waliokuwa wakiangalia mazoezi hayo nje ya uzio walijikuta wakicheka huku wakishangilia.

Helmy ndiye aliyempunguza uzito beki Djuma Shaban kwa kilo tano kutoka 85 na kubaki na 79 hatua ambayo kocha Nasreddine Nabi amechekekelea akidai beki huyo atakuwa bora zaidi msimu ujao.

Wakati Helmy akimfua Morrison, kocha Nabi amefichua anajipanga kufanya kikao maalumu na winga huyo mwenye mbinu za kupangua ukuta.

Nabi alisema anaamini Morrison atakuwa ni mwiba mkali kwa wapinzani msimu ujao, lakini anataka kukaa naye wakiwa wawili tu kumpa mwelekeo wa maisha ndani ya kikosi hicho.

“Sifanyi hivi kwa Morrison peke yake nimeshazungumza na wengine wote ambao wamekuwa wakifika hapa. Ni vizuri akajua maisha yetu hapa na kitu gani tunakitaka kwake na vitu gani hatakiwi kuvifanya hapa,” alisema.

“Kila mmoja anampenda mchezaji mcheshi na hasa Morrison. Huyu ni mchezaji ambaye tumemsajili kwa mahitaji ya timu hasa malengo yetu kwa msimu unaokuja.”

AGEUKA GUMZO

Kama ulikuwa unadhani BM33 kabadilika kwa vituko pole yako, kwani jamaa amegeuka gumzo kwa wachezaji wenzake wakati wa utambulisho na kusababisha Nabi kupigwa butwaa.

Ipo hivi. Wakati wa utambulisho wa wachezaji wapya ilipofika zamu ya Morrison, kocha Nabi alimtaka ajitambulishe ndipo akafanya timu nzima iangue kicheko.

Morrison akiwa uso mkavu alimjibu Nabi; “Jamani... jamani kocha ujitambulishe wewe, mimi ni mwenyeji hapa.” Jambo ambalo lilimfanya Nabi ashindwe uvumilivu na kuangua kicheko.

Wakati kocha Nabi anaendelea kucheka, Morrison aliendelea na utani wake kwa kuwauliza wachezaji aliocheza nao kabla ya kuhamia Simba alikocheza 2020-2022.

“Nyie mliokuwepo eti hamnifahamu jamani...jamani, wewe Fei Toto na wewe hunifahamu.” Jambo lililofanya timu nzima wacheke wakishindwa kuvumilia kuendelea kumsikiliza.

Hata hivyo, ilimlazimu kocha amwambie apunguze utani na ajitambulishe kisha waendelee na mazoezi na akafanya hivyo.

Wachezaji wa timu hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema hadi sasa mchezaji anayeongoza kwa ucheshi na vituko huko kambini ni Morrison anayejichanganya na kila anayemuona mbele yake.

Nje na wachezaji waliyopo Yanga sasa hivi, ambao walicheza naye na wapo na timu nyingine waliyasimulia maisha yake awapo kambini.

Beki wa zamani wa timu hiyo, Juma Makapu ambaye kwa sasa kasajiliwa Ihefu FC alisema Morrison ana vituko na anapokuwepo hapawezi kukosekana mizaha.

“Ni asili yake siyo mambo anayojifunza mnaweza mkaaa na kila mtu akawa na mambo yake anatoka anakotoka anaanza mizaha, naamini huko Avic Town watakuwa na kicheko,” alisema.

Kauli yake iliungwa mkono na Adeyum Saleh ambaye kwa sasa anakipiga Geita Gold “Jamaa ni mcheshi anaweza akaibua jambo hadi ukashangaa, naamini waliyopo kambini watakuwa wanacheka sana.”

Yanga Yapata Mamilioni Mengine kutoka CRDB

 


Clabu ya Yanga Fc Imepata Milioni 25 kutoka kwa Wadhamini wa Wiki ya Yang CRDB

"CRDB Bank imechagua Klabu Kubwa๐Ÿ’ช๐Ÿฝ๐Ÿ”ฐ

@crdbbankplc ➕ ๐—ช๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐— ๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐—ก๐—–๐—›๐—œ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฎ “๐˜‰๐˜บ๐˜ถ๐˜ต๐˜ช๐˜‰๐˜บ๐˜ถ๐˜ต๐˜ช "

#ByutiByuti 
#TimuYaWananchi 
#DaimaMbeleNyumaMwiko....." CRDB Wameandika Wakati Wakionesha Hati ya Malipo.

Kocha wa Yanga Nabi Agombaniwa



TETESI: Klabu ya FAR Rabat ya Morocco inamtaka Kocha Yanga SC Nasreddine Nabi kwa ajili kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck klabuni hapo.


Miamba hiyo ya Morocco ipo tayari kumlipa kocha huyo raia wa Tunisia mshahara wa dola 40,000 (zaidi ya Tsh milioni 93) kwa mwezi ili kumng’oa  kunako klabu ya Yanga.


Source: #KitengeSports

Yanga Yachagua Meneja na Viongozi Wengine Wapya



Raisi wa clabu ya Yanga Eng. Hersi Ally Said Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya Yanga imewateua Saada Kawemba Kuwa Mkurugenzi wa Mashindano na Walter  Harson Kuwa Meneja wa Timu. 


Tazama Taarifa Kamili


USAJILI: MCHEZAJI WA YANGA ASAINI MKATABA MPAKA 2024

 

Mlinzi wa klabu ya Yanga SC Djuma Shabani (29) raia wa DR Congo amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia Mabingwa hao wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara mpaka 2024.