Showing posts with label Football. Show all posts
Showing posts with label Football. Show all posts

Jezi Mpya Za Yanga Msimu Mpya Wa 2023/2024


Kama Ulikua hujaziona jezi mpya za Yanga SC hizi ndio zenyewe.



 Mbunifu wa jezi ya Nyeusi ya Yanga SC kwa msimu huu ameeleza maana ya jezi hiyo huku akijikita kwenye Michoro iliyopo, ameeleza kua;

Jezi ya nyeusi, ukiangalia inamichoro ya 88 na michoro hiyo ilivyokaa imekaa katika mafungu manne ambayo yanamadisha medali nne walizopata Klabu ya Yanga SC


Pia Ameeleza kua ndani ya michoro hiyo kuna Nyota, ambazo zinaeleza kizazi cha nyota au dhahabu ambacho ni Yannga SC ambayo imepitia wakati mzuri mzimu huu.


Kwa Chini kuna nyuzi mzunguko na nembo ambayo ina "Y"; huo mzunguko ulijishikiza katika nembo inawakilisha medali Yanga SC ilizopata na Hiyo Y inamanisha Yanga SC


Je, una maoni gani?

Mbunifu wa jezi ya Yanga SC kwa msimu huu ameeleza maana ya jezi ya njano huku akijikita kwenye Michoro iliyopo, ameeleza kua;

Jezi ya njano maana yake inaelezea matokeo mazuri ya kutokufungwa kwa klabu ya yanga mara nyingi na kutwaa ubigwa


Lakini pia ameeleza kuwa, ukiangalia michoro iliyopo ni ya mchezo mahili wa kupanga matofali ili yasoporomoke, mchezo ambo unahitaji akili na na weredi wa hali ya juu. 


Hiyo inamanisha mipango mathubuti iliyofanywa na Aliyekua kocha wa Yanga SC Nasreddine Nabi ya kuweka vizuri timu hiyo na kuvunja rekodi ya kutwaa ubingwa kwa msimu uliopita




Hizo ndizo jezi za Yanga Msimu huu wa 2023/2024

Man City Vs Arsenal Highlights

 

#EPL Dakika za mwisho kabisa Haaland anaimaliza mechi kwa kuwapachikia Man City goli la 4 dhidi ya Arsenal.


 Man City 4-1 Arsenal

De Bruyne 7',54' 

J.Stones 45+2

Holding 86' 

Haaland 90+5' 


#EPL #ManCity #Arsenal

Diamond Platumz Atanga Kudhamini Mashindano na Wasafibet



Mkurugenzi wa WASAFI BET Diamond Platnumz, ametangaza kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu ya Ndondo CUP kupitia Kampuni yake ya michezo ya kubashiri ya WASAFI BET.


Ndondo Cup ni bidhaa ya Clouds Media inayosimamiwa na Mchambuzi Gwiji Shaffih Dauda. #MillardAyoSPORTS.

Manara Avamia Kambi Ya Simba.



Afisa Muhamasishaji wa Yanga Haji Manara ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la soka nchini TFF, leo ameonekana City Lounge Hotel ambako inasemekana Simba imeweka kambi kwa ajili ya mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.


Haijafahamika Manara alifuata nini hapo, lakini picha za mitandaoni leo zinamuonesha Manara akiwa eneo la mapokezi la Hotel hiyo.


Source: #KitengeSports

MENEJA UWANJA WA MKAPA AONDOLEWA



TAARIFA: Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo, Agosti 9, 2022 amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi kumpangia majukumu mengine Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Bw. Godon Nsajigwa.


Taarifa iliyotolewa na Dkt. Abbasi inasema kuwa Meneja huyo anapangiwa majukumu mengine kwa kushindwa kusimamia matumizi endelevu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Akieleza utekelezaji wa agizo hilo, amesema tayari taratibu zimekwishaanza za kupangiwa majukumu mengine na nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa mara moja.


Source: #KitengeSports

YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL

YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL


Klabu ya Yanga imefikia makubaliano na klabu ya Singida Big Stars juu ya kubadilishana wachezaji Mbrazil Dario Federico Da'Silva JR na Jesus Moloko.


Mbrazil huyo atajiunga na Yanga SC huku Moloko akienda upande wa pili 


Kila kitu kinaenda sawa mezani huku dili hilo likitarajiwa kukamilika kabla ya dirisha kufungwa Agosti 31.


#KitengeSports

𝗑𝗬𝗒𝗧𝗔 π—ͺ𝗔 π—­π—”π— π—”π—‘π—œ π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗔𝗙𝗔π—₯π—œπ—žπ—œ π——π—¨π—‘π—œπ—”



 π—‘𝗬𝗒𝗧𝗔 π—ͺ𝗔 π—­π—”π— π—”π—‘π—œ π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗔𝗙𝗔π—₯π—œπ—žπ—œ π——π—¨π—‘π—œπ—”


#TANZIA: Nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa Iddy Suleiman kibode (Meya) amefariki usiku wa kumkia leo Agosti 8, 2022 katika Hospitali ya Muhimbili. Awali Iddy alilazwa katika hospitali ya Mwananyamala na juzi usiku alihamishiwa Muhimbili.


Idd ni mdogo wa nyota wa zamani, Madaraka Seleman (Mzee wa Kiminyio).


Taratibu za mazishi kitafanyika nyumbani kwao Manzese.


*Source: KitengeSports)

FULL TIME: London Stadium West Ham Utd VS Man City



FULL TIME: #EPL


🏟️ London Stadium


West Ham Utd 0-2 Man City

⚽⚽ Haaland (P) 36' 65' 


Mabingwa watetezi wa ligi kuu England, Man City wameanza vyema kampeni za kutafuta ubingwa wa tatu mfululizo wa ligi hiyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wagonga Nyundo, West Ham United.


Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic

 


Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic

Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Serbia, Dejan Georgijevic kutoka klabu ya NK Domzale.


Georgijevic (28) amesaini mkataba wa mkataba wa miaka miwili kama mapendekezo ya kocha Zoran Maki.


Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa



 Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa


"🚨 Jezi zote ambazo zililetwa awamu ya kwanza zimekwisha. Mzigo mpya utakuwepo madukani ndani ya siku mbili zijazo. #SimbaNaVunjaBei #SimbaWeek #SimbaDay #SimbaDay2022 #NguvuMoja "


Wameandika Simba Katika Mtandao Wa Facebook

TETESI: MAN. UNITED YAGEUKA KWA LEROY SANE

  

TETESI: MAN. UNITED YAGEUKA KWA LEROY SANE


Manchester United inataka kumsajili Winga wa Bayern Munich, Leroy Sane na imeanza mazungumzo na Bayern


Sane ambaye amewahi kuichezea Man. City ana mkataba wa miaka mitatu kutumikia Bayern.

Hizi Hapa Jezi Mpya Za Simba SC 2022/23

  Hizi Hapa Jezi Mpya Za Simba SC 2022/23








MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"

 

MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"


Aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema ameshiriki kwenye Siku ya Mwananchi kama mshereheshaji (MC) na sio kama mhamasishaji.

Manara amesema hayo baada ya kutambulisha kikosi cha Yanga mwaka 2022/2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.

  

Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.

TAARIFA: Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa ofisa wa klabu hiyo Haji Manara.


Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo.


Naye Mhandisi Said amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na Ibara ya 16(1)(a) ya Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.


Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF tayari amepelekewa mashtaka hayo, walala mikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati hiyo kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo.




FULL TIME: YANGA SC 0-2 VIPERS FC



FULL TIME: YANGA SC 0-2 VIPERS FC


🏟️ Benjamin Mkapa


YANGA SC 0-2 VIPERS FC

⚽ Karisa 1'

⚽ Anukani 65'


Shughuli imemalizika katika dimba la Benjamin Mkapa, Vipers wameharibu siku ya MWANANCHI baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji wao Yanga SC.


Magoli ya wageni yamefungwa na Milton Karisa na Bright Anukani.


UKWELI KUSU JEZI ZA SIMBA KUKWAMA BANDARINI KISA UBORA

 


 UKWELI KUSU JEZI ZA SIMBA KUKWAMA BANDARINI KISA UBORA


Huenda Mashabiki wa Klabu ya Simba wakakosa nafasi ya kuwa na Jezi maalum wakati wa Tamasha la Simba ‘Simba Day’ siku ya Jumatatu ‘Agosti 08’ Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Hadi sasa Simba SC haijatambulisha jezi mpya za Msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema hadi sasa klabu hiyo pamoja na Mbunifu na Muuzaji Rasmi wa Vifaa vya Michezo vya Klabu hiyo kampuni ya Vunja Bei wanaendelea kupambana na changamoto ambazo zimesababisha jezi za msimu ujao kutoka kwa wakati.

Ahmed Ally ameweka wazi suala hilo alipofanyiwa mahojiano na Kituo cha Wasafi FM, leo Ijumaa ‘Agosti 08’ kupitia Kipindi cha Sports Arena kilichorushwa asubuhi.

“Jezi hazijazuiwa bandarini na (TBS) kwa sababu ya ubora hafifu wala si kwa sababu wameshindwa kuzilipia kodi kama baadhi ya watu wanavyosema,”

“Sio kawaida na sio sawa kutokutangaza Jezi zetu mpaka Leo! Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida kimesababisha kuchelewa na sio kwamba zimekwama bandarini”

“Mabadiliko ya Mdhamini mchakato ulianza mwezi wa 6 ukachukua muda, mnakubaliana lakini kesho mdhamini anaibuka na mawazo mengine.”

“Kama tungebaki na mdhamini aliyepita tungekuwa na Jezi mpya mapema sana” amesema Ahmed.

Waarabu wamuwekea Sakho milioni 800

 




Waarabu wamuwekea Sakho milioni 800


 KLABU ya wananchi ya Raja Athletic ya Morocco iko katika hesabu kali ikipigania saini ya winga wa Simba, Pape Sakho na fedha ambayo wameitaja kupata saini hiyo ni kama mtego kwa Wekundu wa Msimbazi.

Raja kupitia rais wao, Aziz El Badraoui wamepania kunasa saini ya winga huyo raia wa Senegal na tayari wameitengea Simba Dola 350,000 (takriban Sh815 milioni) ili wainase saini ya Sakho ambaye hivi karibuni alinyakua kiatu cha mfungaji wa bao bora la michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kunyakua kiatu hicho, mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alikaririwa akisema tayari wanazo ofa kibao za wachezaji wao kutakiwa na timu mbalimbali Afrika akiwemo Sakho.

Inaelezwa Raja wameshafanya ushawishi kwa Sakho ambaye naye amewasukumia kwa mabosi wa klabu hiyo ili wamalizane, lakini mtego ni bado nyota huyo ana mkataba na Wekundu hao huku ofa hiyo ikiwa moja tu kati ya zingine nzuri ambazo Simba inazipima.

Badraoui ameliambia Mwanaspoti kwa njia ya simu, wamevutiwa na Sakho na wako katika hatua nzuri ya kuwasilisha rasmi yao kwa wekundu hao baada ya kuongea kwa njia ya simu kupima kama wanaweza kumwachia mshindi huyo wa tuzo ya mfungaji wa bao bora la msimu la CAF.

“Tulianza kumfuatilia kwa muda mrefu Pape (Sakho) ni mchezaji mdogo mwenye kipaji, hapa Raja tunahitaji wachezaji wa kiwango kama hicho tutawasiliana kwa ukamilifu na Simba hivi karibuni, mchezaji hana tatizo,” alisema.

ADVERTISEMENT

Wakati uongozi ukijipanga hivyo naye kocha wa timu hiyo mkongwe Faouzi Benzarti amekuwa akifuatilia taarifa zaidi za ubora za Sakho katika kujiridhisha zaidi.

Mwanaspoti linafahamu kwamba Faouzi ambaye ni kocha wa zamani wa Γ‰toile du Sahel na Wydad Athletic amekuwa katika mawasiliano na makocha ambao wamewahi kukutana na Sakho akitaka kujua ubora wake zaidi.

Simba bado haijafanya uamuzi wa kipi ifanye katika ofa walizonazo juu ya Sakho huku pia Al Hilal ya Sudan ikipambana kunasa saini ya winga huyo.

BAYERN MUNICH VS EINTRACHT FRANKFURT



BAYERN MUNICH VS EINTRACHT FRANKFURT

 FULL TIME: #Bundesliga


🏟️ Deutsche Bank Park


EINTRACHT FRANKFURT 1-6 BAYERN MUNICH


⚽️ Joshua Kimmich 4' H

⚽️ Benjamin Pavard 10'

⚽️ Sadio Mane 29'

⚽️ Jamal Musiala 35' 83'

⚽️ Serge Gnabry 43'

⚽️ Randal Kolo Muani 64'


Bayern Munich imeshusha mvua ya magoli 6-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt katika dimba la Deutsche Bank Park dhidi ya Frankfurt.


The Bavarians wanafungua pazia la ligi kwa kishindo licha ya kuondoka kwa mashine ya magoli Robert Lewandowski.


Moriso Ashtukiwa, Apewa Siku 14

 

BERNARD Morrison ameanza kazi rasmi Yanga na leo akiingia siku ya nne mazoezini, lakini kocha mmoja fundi wa mazoezi ameshtukia kitu kwa winga huyo Mghana kisha akamtengea siku 14 za kazi nzito.

Kocha aliyemshtukia BM33 ni Helmy Gueldich ambaye ni kocha wa mazoezi ya viungo aliyeangalia ubora wa mshambuliaji huyo kisha akagundua kwamba jamaa hakufuata sawasawa ratiba ya mazoezi waliyomtumia.

Helmy hata hivyo ameliambia Mwanaspoti kwamba Morrison yuko nusu fiti - nusu unga, lakini ndani ya wiki mbili tu atakuwa katika daraja lingine la ubora.

Kocha huyo alisema katika ratiba ya wiki ya kwanza Morrison atakuwa na kazi ngumu ambayo itamsaidia baadaye kurudisha ubora.

“Tulimpatia ratiba mapema kabla ya kujiunga alitakiwa kuifanya kwa ukamilifu lakini nimemuangalia naona hakuifuata sawasawa ila atakuwa sawa,” alisema Helmy ambaye bado anahitajika Chama cha Soka Tunisia.

“Ni mchezaji mzuri (Morrison) sio mbaya kwa hali aliyokuja nayo kitu kibaya angekuwa hajafuata kabisa lakini tuna muda wa kumrudisha katika mstari.”

Juzi Morrison alikimbizwa mazoezini Yanga akizunguka peke yake pembeni kisha akasimama na kulalamika akiongea kwa Kiswahili akisema: “Huyu jamaa anaiua huyu’ kauli ambayo mashabiki waliokuwa wakiangalia mazoezi hayo nje ya uzio walijikuta wakicheka huku wakishangilia.

Helmy ndiye aliyempunguza uzito beki Djuma Shaban kwa kilo tano kutoka 85 na kubaki na 79 hatua ambayo kocha Nasreddine Nabi amechekekelea akidai beki huyo atakuwa bora zaidi msimu ujao.

Wakati Helmy akimfua Morrison, kocha Nabi amefichua anajipanga kufanya kikao maalumu na winga huyo mwenye mbinu za kupangua ukuta.

Nabi alisema anaamini Morrison atakuwa ni mwiba mkali kwa wapinzani msimu ujao, lakini anataka kukaa naye wakiwa wawili tu kumpa mwelekeo wa maisha ndani ya kikosi hicho.

“Sifanyi hivi kwa Morrison peke yake nimeshazungumza na wengine wote ambao wamekuwa wakifika hapa. Ni vizuri akajua maisha yetu hapa na kitu gani tunakitaka kwake na vitu gani hatakiwi kuvifanya hapa,” alisema.

“Kila mmoja anampenda mchezaji mcheshi na hasa Morrison. Huyu ni mchezaji ambaye tumemsajili kwa mahitaji ya timu hasa malengo yetu kwa msimu unaokuja.”

AGEUKA GUMZO

Kama ulikuwa unadhani BM33 kabadilika kwa vituko pole yako, kwani jamaa amegeuka gumzo kwa wachezaji wenzake wakati wa utambulisho na kusababisha Nabi kupigwa butwaa.

Ipo hivi. Wakati wa utambulisho wa wachezaji wapya ilipofika zamu ya Morrison, kocha Nabi alimtaka ajitambulishe ndipo akafanya timu nzima iangue kicheko.

Morrison akiwa uso mkavu alimjibu Nabi; “Jamani... jamani kocha ujitambulishe wewe, mimi ni mwenyeji hapa.” Jambo ambalo lilimfanya Nabi ashindwe uvumilivu na kuangua kicheko.

Wakati kocha Nabi anaendelea kucheka, Morrison aliendelea na utani wake kwa kuwauliza wachezaji aliocheza nao kabla ya kuhamia Simba alikocheza 2020-2022.

“Nyie mliokuwepo eti hamnifahamu jamani...jamani, wewe Fei Toto na wewe hunifahamu.” Jambo lililofanya timu nzima wacheke wakishindwa kuvumilia kuendelea kumsikiliza.

Hata hivyo, ilimlazimu kocha amwambie apunguze utani na ajitambulishe kisha waendelee na mazoezi na akafanya hivyo.

Wachezaji wa timu hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema hadi sasa mchezaji anayeongoza kwa ucheshi na vituko huko kambini ni Morrison anayejichanganya na kila anayemuona mbele yake.

Nje na wachezaji waliyopo Yanga sasa hivi, ambao walicheza naye na wapo na timu nyingine waliyasimulia maisha yake awapo kambini.

Beki wa zamani wa timu hiyo, Juma Makapu ambaye kwa sasa kasajiliwa Ihefu FC alisema Morrison ana vituko na anapokuwepo hapawezi kukosekana mizaha.

“Ni asili yake siyo mambo anayojifunza mnaweza mkaaa na kila mtu akawa na mambo yake anatoka anakotoka anaanza mizaha, naamini huko Avic Town watakuwa na kicheko,” alisema.

Kauli yake iliungwa mkono na Adeyum Saleh ambaye kwa sasa anakipiga Geita Gold “Jamaa ni mcheshi anaweza akaibua jambo hadi ukashangaa, naamini waliyopo kambini watakuwa wanacheka sana.”