Showing posts with label TFF Tanzania. Show all posts
Showing posts with label TFF Tanzania. Show all posts

TFF NA ACT WAZALENDA WAMINYANA - KANUNI MPYA

 


Kufuatia taarifa ya Bodi ya Ligi juu ya maboresho ya kanuni ambapo imeweka marufuku kwa mchezaji kuingia mkataba binafsi wa udhamini na mshindani kibiashara wa mdhamini mkuu wa Ligi, Chama cha ACT Wazalendo kimeshangazwa sana kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kupitia bodi ya Ligi kwa kukubali kuingiza masharti haya katika wakati ambao nchi inapambana kuona michezo inaenda kuinua maisha ya vijana wengi kwa kutoa ajira na kukuza maslahi ya wachezaji.


Aidha ACT Wazalendo kupitia kwa Kamati ya Kuisimamia Serikali ya Wasemaji wa Kisekta (Baraza Kivuli la Mawaziri) imesema “tunaungana” na wadau wengine kupinga maboresho hayo ya kanuni kwasababu zifuatazo:-


i) Kanuni hii inawanyima wachezaji uhuru na haki binafsi katika kujitafutia kipato. Mchezaji ni raia wa kawaida anayeweza kushiriki kwenye matangazo binafsi na kampuni au taasisi yoyote ambayo haikiuki haki za kipekee (exclusive rights) za Mdhamini Mkuu wa Ligi.


ii) TFF katika kununi ya 16 (1.4, 5,6) imeweka makatazo na utaratibu wa matangazo yasiyokuwa ya Mdhimini Mkuu ambapo vifungu vyote vimezuia maeneo ya uwanja pamoja na matumizi ya nembo ya mdhamini Mkuu kwenye vifaa vya kuchezea vya timu husika. Ni wazi kwamba haki zote kwa mdhamini mkuu zimeorodheshwa kuongeza kifungu hiki ni kukandamiza maslahi ya wachezaji. 


iii) Maboresho ya kanuni hayajatoa tafsiri ya shughuli zitakazo chukuliwa kuwa ni kuingiliana na zile za Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu. Hii inaweza kutoa tafsiri tofauti tofauti au inaweza kutumika vibaya kuzuia matangazo kwa wachezaji.


iv) Kanuni imekuja bila kuchukua uzoefu kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kusimamia haki na maslahi ya wachezaji linapoja suala la udhamini. Uzoefu wa wachezaji wakubwa Duniani wamekuwa wakiingia mikataba binafsi na kampuni tofauti tofauti ambazo zinamgongano wa kimaslahi wa karibu. Mdhamani Mkuu hawezi kupewa haki ya Uhodhi hata kwa maisha ya wachezaji. Hii haikubaliki.


Hivyo basi, ACT Wazalendo kupitia kwa Msemaji wa Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo tunaitaka TFF na Bodi ya Ligi kuondoa marekebisho haya mapya ili kulinda maslahi ya wachezaji.


Pili, tunaitaka kuwepo kwa ushirikishaji katika masuala yote ya michezo yanayohusu pande mbalimbali. 



Source: KitengeSpo

TFF YATOA MAJINA YA WATAKAO CHEZESHA MPIRA NGAO YA JAMII



Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ngao ya Jamii 2022


@yangasc  @simbasctanzania @azamsports2 @ligikuu @nbc_tanzania



RAISI WA FIFA ATUA TANZANIA



Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) Gianni Infantino ametua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kwa kuhudhuria mkutano wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) unaofanyika Arusha.


Ameongozana mwamuzi wa kimataifa mstaafu Pierluigi Collina.


MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"

 

MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"


Aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema ameshiriki kwenye Siku ya Mwananchi kama mshereheshaji (MC) na sio kama mhamasishaji.

Manara amesema hayo baada ya kutambulisha kikosi cha Yanga mwaka 2022/2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.

  

Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.

TAARIFA: Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa ofisa wa klabu hiyo Haji Manara.


Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo.


Naye Mhandisi Said amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na Ibara ya 16(1)(a) ya Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.


Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF tayari amepelekewa mashtaka hayo, walala mikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati hiyo kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo.




LIGI KUU BARA - Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Imetoa Ratiba kwa Msimu wa 2022/23



Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetoa ratiba kwa msimu wa 2022/23 ambapo pazia litafunguliwa rasmi agosti 13 (ngao ya hisani ) kisha Agosti 15 michezo ya ligi kuu itaanza rasmi.


Swipe 👉🏿 kuona ratiba nzima. #WekaManeno











Mtibwa Sugar Bingwa Tena Ligi kuu U-20



Mtibwa sugar imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa msimu huu wa 2021/2022 baada ya kuifunga timu ya Mbeya Kwanza kwa magoli goli 4-1 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Julai 17, 2022 majira ya 11:00 jioni Katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Hii ni mara ya nne mfululizo kwa timu hiyo kubeba Kombe hilo la ligi kuu ya vijana (U-20) katika mashindano yanayo andaliwa na kusimamiwa na TFF.

Kocha wa Mtibwa Sugar Awadh Juma alisema “tunamshukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena, niipongeze timu yangu kwa kufanya vizuri na niipongeze TFF kwa maandalizi mazuri na kuratibu vizuri ligi hii kwani imekuwa na ushindani wa aina yake ukilinganisha na mwaka uliopita. Tumeona vipaji vingi na vichanga ambavyo vikiendelezwa vitakuwa na mchango mkubwa kwa vilabu vyetu.”

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Ezekiel Eusebio dk 20, Ladack Chasambi dk 45, Said Mkopi dk 84 na Omary Suleiman dk 90 wakati goli pekee la Mbeya Kwanza likifungwa na Willie Thobias dk ya 68.

Timu ya Mtibwa sugar imefanikiwa kutoa golikipa bora ambaye ni Razack Shekimweli, Mchezaji bora Ladack Chadambi na kocha Bora wa ligi akiwa ni Awadh juma. Tuzo zingine zilizotolewa ni mwamuzi bora iliyochukuliwa na Kelvin Martin, mwamuzi msaidizi ikibebwa na Tumaini Kimaro.

Mchezo mwingine uliopigwa kwenye fainali hizo ni mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao ulimalizika kwa Azam FC kuifunga Coastal Union kwa penati 4-3 baada ya dk 90 kutamatika kwa sare ya 1-1