Showing posts with label Simba SC. Show all posts
Showing posts with label Simba SC. Show all posts

Al Hilal Yawashitaki Wachezaji Wanaotajwa Simba SC Azam FC



Al Hilal Wamewashitaki wachezaji watatu waliovunja mkataba ka klabu hiyo bila kufuata utaratibu.


Wachezaji waliositisha mikataba hiyo ni Fabrice Ngoma anayehusishwa Simba, Lamin Jarjou akitajwa Azam FC pamoja na Ibrahim Imoro ambaye bado haijajulika anataka kutimkia timu gani.


Ngoma anadaiwa kusitisha mikataba wake kinyume na taratibu na hiyo kutokuwa na mwanzo mbaya ndani ya timu hiyo kutokana na kuwa na majeruhi wa mara kadhaa.


Kiungo huyo tayari yupo Dar es Salaam akisubiri barua yake ya kumalizana na Al Hilal na wakati wowote anaweza kusaini Simba tofauti na ilivyozushwa kuwa atasaini Yanga au Azam FC.


Wachezaji hao ambao wapo chini ya kocha Florent Ibenge wako njiapanda kwani hatima ya maombi yao ya kusitisha mikataba haijafika tamati.

Mchezaji Aliyesajiliwa Simba Sc ni Mauzauza

 


Ngoma Siyo kiwango cha simba sc, ni kama Sawadogo tu.


"Kwa kiwango cha Fabrice Ngoma na malengo ya Simba nadhani pale wamezika tu pesa zao kama ilivyokuwa kwa Sawadogo,nadhani Simba wangetafuta mchezaji mungine tu lakini Kwa Ngoma wametupa pesa zao" @alexngereza._


Mbali na hayo zipo tetesi ni kuwa Ngoma alikua hajamalizana na mabosi wake na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kufunguliwa kesi katika vyombo vinavyohusika na wachezaji. 

mechi za simba club bingwa 2023

mechi za simba club bingwa 2023 



Ijumaa hii mnyama @simbasctanzania atakuwa dimba la Mohammed V nchini Morocco kukipiga na Wydad Casablanca katika mechi ya mkondo wa pili robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mnyama ataingia katika mchezo huu akiwa na mtaji wa goli moja alilopata mechi ya kwanza.


#cafcl

Timu ya Simba SC Ikiwasili Casablanca

 Matukio katika Picha







Soka: Wachezaji 9 Wa Simba SC 9️⃣ wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars



 Wachezaji wetu 9️⃣ wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars πŸ‡ΉπŸ‡Ώ kujiandaa na michezo ya kufuzu CHAN.

▪️ Aishi Manula

▪️ Beno Kakolanya

▪️ Shomari Kapombe

▪️ Mohamed Hussein

▪️ Kennedy Juma

▪️ Jonas Mkude

▪️ Mzamiru Yassin

▪️ Kibu Denis

▪️ Habibu Kyombo






#NguvuMoja

Mpole, Sitofahamu Chezo wa Simba Sc Vs Geita Gold



Kuelekea mchezo wa kesho kati ya Geita Gold na Simba SC, Geita Gold ipo kwenye sintofahamu juu ya mshambuliaji George Mpole ambaye hayupo kambini na amethibitisha kuwa ana ofa kutoka nje ya Nchi anazishughulikia na mambo yakikaa sawa ataondoka.


Katika mahojiano na EFM SPORT HQ mfungaji huyo Bora wa NBCPL 2021/22 amethibitisha kuwa mkataba wake na Geita Gold umekwisha.


Source: #KitengeSports

Manara Avamia Kambi Ya Simba.



Afisa Muhamasishaji wa Yanga Haji Manara ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la soka nchini TFF, leo ameonekana City Lounge Hotel ambako inasemekana Simba imeweka kambi kwa ajili ya mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.


Haijafahamika Manara alifuata nini hapo, lakini picha za mitandaoni leo zinamuonesha Manara akiwa eneo la mapokezi la Hotel hiyo.


Source: #KitengeSports

Simba Day: Hali Ilivyo Uwanja wa Benjamin Mkapa

 Kutoka majukwaa ya Benjamin Mkapa Stadium #SimbaDay2022







 



𝗑𝗬𝗒𝗧𝗔 π—ͺ𝗔 π—­π—”π— π—”π—‘π—œ π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗔𝗙𝗔π—₯π—œπ—žπ—œ π——π—¨π—‘π—œπ—”



 π—‘𝗬𝗒𝗧𝗔 π—ͺ𝗔 π—­π—”π— π—”π—‘π—œ π—¦π—œπ— π—•π—” 𝗔𝗙𝗔π—₯π—œπ—žπ—œ π——π—¨π—‘π—œπ—”


#TANZIA: Nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa Iddy Suleiman kibode (Meya) amefariki usiku wa kumkia leo Agosti 8, 2022 katika Hospitali ya Muhimbili. Awali Iddy alilazwa katika hospitali ya Mwananyamala na juzi usiku alihamishiwa Muhimbili.


Idd ni mdogo wa nyota wa zamani, Madaraka Seleman (Mzee wa Kiminyio).


Taratibu za mazishi kitafanyika nyumbani kwao Manzese.


*Source: KitengeSports)

CAF YATOA RATIBA YA LIGI 2022/23


CAF YATOA RATIBA YA LIGI 2022

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya timu zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu wa 2022/23 huku Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ ikiwakilishwa na Simba, Yanga (Ligi ya Mabingwa Afrika) na timu zote zitaanzia hatua ya awali na Kombe la Shirikisho zitakuwepo Geita Gold na Azam FC ambayo ni timu pekee πŸ‡ΉπŸ‡Ώ itaanzia hatua inayofuata. 


Droo itafanyika kesho Agosti 9 jijini Cairo, Misri. 




Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic

 


Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic

Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Serbia, Dejan Georgijevic kutoka klabu ya NK Domzale.


Georgijevic (28) amesaini mkataba wa mkataba wa miaka miwili kama mapendekezo ya kocha Zoran Maki.


Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa



 Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa


"🚨 Jezi zote ambazo zililetwa awamu ya kwanza zimekwisha. Mzigo mpya utakuwepo madukani ndani ya siku mbili zijazo. #SimbaNaVunjaBei #SimbaWeek #SimbaDay #SimbaDay2022 #NguvuMoja "


Wameandika Simba Katika Mtandao Wa Facebook

Hizi Hapa Jezi Mpya Za Simba SC 2022/23

  Hizi Hapa Jezi Mpya Za Simba SC 2022/23








UKWELI KUSU JEZI ZA SIMBA KUKWAMA BANDARINI KISA UBORA

 


 UKWELI KUSU JEZI ZA SIMBA KUKWAMA BANDARINI KISA UBORA


Huenda Mashabiki wa Klabu ya Simba wakakosa nafasi ya kuwa na Jezi maalum wakati wa Tamasha la Simba ‘Simba Day’ siku ya Jumatatu ‘Agosti 08’ Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Hadi sasa Simba SC haijatambulisha jezi mpya za Msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema hadi sasa klabu hiyo pamoja na Mbunifu na Muuzaji Rasmi wa Vifaa vya Michezo vya Klabu hiyo kampuni ya Vunja Bei wanaendelea kupambana na changamoto ambazo zimesababisha jezi za msimu ujao kutoka kwa wakati.

Ahmed Ally ameweka wazi suala hilo alipofanyiwa mahojiano na Kituo cha Wasafi FM, leo Ijumaa ‘Agosti 08’ kupitia Kipindi cha Sports Arena kilichorushwa asubuhi.

“Jezi hazijazuiwa bandarini na (TBS) kwa sababu ya ubora hafifu wala si kwa sababu wameshindwa kuzilipia kodi kama baadhi ya watu wanavyosema,”

“Sio kawaida na sio sawa kutokutangaza Jezi zetu mpaka Leo! Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida kimesababisha kuchelewa na sio kwamba zimekwama bandarini”

“Mabadiliko ya Mdhamini mchakato ulianza mwezi wa 6 ukachukua muda, mnakubaliana lakini kesho mdhamini anaibuka na mawazo mengine.”

“Kama tungebaki na mdhamini aliyepita tungekuwa na Jezi mpya mapema sana” amesema Ahmed.

Waarabu wamuwekea Sakho milioni 800

 




Waarabu wamuwekea Sakho milioni 800


 KLABU ya wananchi ya Raja Athletic ya Morocco iko katika hesabu kali ikipigania saini ya winga wa Simba, Pape Sakho na fedha ambayo wameitaja kupata saini hiyo ni kama mtego kwa Wekundu wa Msimbazi.

Raja kupitia rais wao, Aziz El Badraoui wamepania kunasa saini ya winga huyo raia wa Senegal na tayari wameitengea Simba Dola 350,000 (takriban Sh815 milioni) ili wainase saini ya Sakho ambaye hivi karibuni alinyakua kiatu cha mfungaji wa bao bora la michuano inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kunyakua kiatu hicho, mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alikaririwa akisema tayari wanazo ofa kibao za wachezaji wao kutakiwa na timu mbalimbali Afrika akiwemo Sakho.

Inaelezwa Raja wameshafanya ushawishi kwa Sakho ambaye naye amewasukumia kwa mabosi wa klabu hiyo ili wamalizane, lakini mtego ni bado nyota huyo ana mkataba na Wekundu hao huku ofa hiyo ikiwa moja tu kati ya zingine nzuri ambazo Simba inazipima.

Badraoui ameliambia Mwanaspoti kwa njia ya simu, wamevutiwa na Sakho na wako katika hatua nzuri ya kuwasilisha rasmi yao kwa wekundu hao baada ya kuongea kwa njia ya simu kupima kama wanaweza kumwachia mshindi huyo wa tuzo ya mfungaji wa bao bora la msimu la CAF.

“Tulianza kumfuatilia kwa muda mrefu Pape (Sakho) ni mchezaji mdogo mwenye kipaji, hapa Raja tunahitaji wachezaji wa kiwango kama hicho tutawasiliana kwa ukamilifu na Simba hivi karibuni, mchezaji hana tatizo,” alisema.

ADVERTISEMENT

Wakati uongozi ukijipanga hivyo naye kocha wa timu hiyo mkongwe Faouzi Benzarti amekuwa akifuatilia taarifa zaidi za ubora za Sakho katika kujiridhisha zaidi.

Mwanaspoti linafahamu kwamba Faouzi ambaye ni kocha wa zamani wa Γ‰toile du Sahel na Wydad Athletic amekuwa katika mawasiliano na makocha ambao wamewahi kukutana na Sakho akitaka kujua ubora wake zaidi.

Simba bado haijafanya uamuzi wa kipi ifanye katika ofa walizonazo juu ya Sakho huku pia Al Hilal ya Sudan ikipambana kunasa saini ya winga huyo.

Simba Alamba Dili Juu Ya Dili



 "CRDB ni official Simba Day partner."


"CRDB wameona ni muhimu kuwekeza kwenye michezo na wamechagua Simba sababu wanaona ukubwa wa Simba."


"Tunawashukuru CRBD kuwekeza kwenye Simba Day, najua huu ni mwanzo. Tunatamani siku moja kuwaona hata kwenye jezi. Baada ya Simba Day kuna CRDB Marathon na sisi tutashiriki."


"Hata kama kampuni haina rangi nyekundu, tuko tayari kufanya nayo kazi, tunaheshimu brand, hatuwezi kubadilisha rangi ya logo yao."- CEO Barbara Gonzalez. #SimbaNaCRDB #SimbaWeek #SimbaDay #SimbaDay2022 #NguvuMoja

Kocha Wa Simba Ashabikia Suala la Ratiba Ligi Kuu

 

Kocha wa Simba, Zoran Maki amesema ratiba ya Ligi Kuu Bara imekuwa rafiki kwao kutokana na kucheza mechi tatu za kwanza katika uwanja wa nyumbani ambao upo na mazingira mazuri haswa eneo la kuchezea.

Zoran amesema  wanatakiwa kuanza vizuri katika mechi hizo kwa kukusanya pointi zote tisa ili ikianza ratiba ya kucheza mechi za ugenini wanakupa na kitu wamekifanya tayari.

Amesema kuanza Ligi kwa kupata ushindi katika mechi tatu za awali maana yake watakuwa wametengeza morali kubwa kwa wachezaji wake hata wakitoka katika mechi za nje.

“Ukiangalia msimu uliopita miongoni mwa sababu iliyochangia Simba kushindwa kufanya vizuri kutopata matokeo mazuri katika mechi nyingi za nyumbani kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao,” amesema Zoran na kuongeza;

“Kwahiyo katika hizi mechi tatu za nyumbani tutaweka mipango ya kupata ushindi na hilo linawezekana kutokana na maandalizi mazuri waliyopata wachezaji,”

“Ukiangalia aina ya timu ambazo tunakwenda kukutana nazo ni nzuri na naamini zitatupa ushindani wa kutosha, tunaelewa hilo na tupo tayari kupambana nalo.”

Katika mechi tatu za awali kwenye Ligi Kuu Bara Simba itaanzia nyumbani dhidi ya Geita Gold, Kagera Sugar na KMC.

FT: Simba Sc Vs Al-Kholood - Simba Yapata Ushindi



Kikosi cha Simba kimecheza mechi ya mwisho ya kirafiki nchini Misri leo dhidi ya Al-Kholood kutoka Saudi Arabia na kushinda mabao 2-0 yakifungwa na Gadiel Michael na Augustine Okrah. Timu hiyo inatarajiwa kurejea Dar Agosti 4 kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day.


#mwanaspoti

#mwanaspotiupdates 

#tunawezeshataifa

SIMBA YAPATA MABILIONI KUTOKA M-BET

 

Sehemu Ya Maelezo ya Mkurugenzi wa masoko M-Bet,


"M-Bet ni kampuni namba moja ya michezo ya kubashiriki sasa tunashirikiana na klabu namba moja Tanzania."


"Tunaamini kama M-Bet tukishirikiana na Simba tutajitangaza ndani na nje ya Tanzania."


"Mwaka wa kwanza - Bil 4.670

Mwaka wa pili - Bil 4.925

Mwaka wa tatu - Bil 5.205

Mwaka wa nne - Bil 5.514

Mwaka wa tano - Bil 5.853


Jumla ni Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000."- Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi. #SimbaNaMBet #SimbaWeek #SimbaDay #NguvuMoja

Simba Sc Kucheza na Al-Kholood Misri



Klabu Simba imethibitisha kuwa itacheza mchezo wake wa nne wa kirafiki Mjini Ismailia, Misri dhidi ya klabu ya Al-Kholood.


Simba SC imecheza mechi tatu za kirafiki mpaka sasa Nchini Misri ikishinda mmoja, sare moja na kipigo mara Moja.


#Michezo