Simba Kufanya Usajili Wa Zimamoto
Yanga Yanasa Saini Ya Kiungo Mwingine
Yanga Yanasa Saini Ya Kiungo Mwingine
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo Pacรดme Zouzoua raia wa Ivory coast Kutoka Asec mimosas.
Pacรดme Zouzoua amewasili leo asubuhi nchini Tanzania kutokea Ivory coast akiwa na wakala wake, Wameshakamilisha zoezi la kusaini mkataba mchana huu salamander tower.
Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kupewa namba 10
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao
๐จ OFFICIAL & CONFIRMED:
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kulia Kouassi Attohoula Yao kutoka Asec kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Yao (26) ๐ฎ๐ช anahesabika kuwa beki bora wa kulia pia na ubora wa kucheza kama winga mshambuliaji na kupiga krosi za mabao.
MFAHAMU KOUASSI ATTOHOULA.
Jina kamili: KOUASSI ATTOHOULA YAO.
Watu wa nyumbani kwao wanapenda kumuita kwa jina la KOUASSI ATTOHOULA YAO.
Raia wa Ivory coast
....Alizaliwa Anyama,Ivory coast
mnamo Dec 20,1996 (Age 26)
Ana urefu wa 1.68m.
Wakala :VV Consulting.
⬛ Nafasi anayochezea ni beki wa kulia
.... Nafasi nyingine anayoweza kucheza ni beki wa kushoto/winga.
Alianza maisha ya soka kwenye akademi ya Mimosas na kuitumikia akademi hiyo kwenye vikosi vya U17 na U19.
✅Julai 1,2017 akasajiliwa na klabu ya Williamsville ya nchini humo akitumikia kwa miaka miwili.
✅Akauzwa kwenda klabu ya O.Khouribga ya nchini Morocco Jan 16,2019 aliitumikia kwa miezi 6 kisha akatolewa kwa mkopo kwenda kwenye klabu ya Kawkab Marrak mnamo Julai 17,2019.
✅ Mnamo Sep 15,2019 baada ya mkataba wa mkopo kuisha alirejea kwenye klabu yake ya O.Khouribga.
Na mkataba wake ndani ya klabu hiyo uliisha miezi miwili baade.
✅๐กNdipo akajiunga tena na klabu ya Asec Mimosas ya Wakubwa Nov 9,2020.
MASHINDANO YA CAF KAMA MCHEZAJI
✅ Amecheza jumla ya mechi 35 ya mashindano haya ya CAF ngazi ya vilabu.
...CAFCL
Amecheza mechi 27, kati ya hizo ni mechi 5 tu alitokea benchi.
..... CAFCC
Amecheza mechi 8, kati ya hizo ni mechi 1 tu alitokea benchi.
Akiwa ligi ya Morocco alicheza mechi 9 na kufunga goli 1.
Aug 27 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 25,miezi 8 na siku 7 alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast chini ya kocha Jean Louis Gasset.
Mpaka sasa ameichezea hiyo ya taifa (michuano ya CHAN,na timu ya taifa ya pamoja) michezo 6.
Aliwahi kuwa beki bora wa msimu wa ligi kuu Ivory Coast 2021/22.
Alikuwa miongoni kwa walioiunda kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Ivory Coast kwenye msimu wa 2021/22 na msimu uliopita wa 2022/23
Mshindi wa Makombe mawili ya Ligi kuu Ivory Coast
Mshindi wa Makombe mawili ya FA.
Klabu Ya Simba SC Tanzania imemtambulisha rasmi Fabrice Ngoma.
... || BREAKING
Klabu Ya Simba SC Tanzania imemtambulisha rasmi Fabrice Ngoma.
Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma kutoka kwa vigogo wa Sudan, Al Hilal Omdurman kwa mkataba wa miaka miwili.
Ngoma (29) raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kati akiwa na uzoefu na michuano ya Kimataifa amewahi kuvitumikia vilabu vya AS Vita ya DRC na Raja Casablanca ya Morocco.
MFAHAMU FABRICE NGOMA
Amesajiliwa na klabu ya Simba akiwa huru (Free agent) baada ya mkataba wake na Al Hilal kumalizika 1 July 2023.
◉ Born — 22 January 1994 (29)
◉ Citizenship — Dr Congo ๐จ๐ฉ
◉ Height — 1,88 m (feet 6.2in)
◉ Position — Central midfielder
Mwamba ameupiga katika klabu mbalimbali kama ifuatavyo ;
◉ 22/23 — Al Hilal ๐ธ๐ฉ
◉ 22/23 — Al Fahaleel SC ๐ฆ๐ช
◉ 19/20 — Raja Casablanca ๐ฒ๐ฆ
◉ 17/18 — AS Vita ๐จ๐ฉ
◉ 16/17 — Ifeanyi Ubah ๐ณ๐ฌ
◉ 15/16 — Itancheite ๐จ๐ฉ
Stats career
๐ 05 — Al Hilal ๐ธ๐ฉ
๐ 04 — Al Faheel SC๐ฆ๐ช
๐ 88 — Raja Casablanca ๐ฒ๐ฆ
๐ 23 — AS Vita ๐จ๐ฉ
๐ 58 — Ifeanyi Ubah ๐ณ๐ฌ
๐ Amejiunga na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
Al Hilal Yawashitaki Wachezaji Wanaotajwa Simba SC Azam FC
Al Hilal Wamewashitaki wachezaji watatu waliovunja mkataba ka klabu hiyo bila kufuata utaratibu.
Wachezaji waliositisha mikataba hiyo ni Fabrice Ngoma anayehusishwa Simba, Lamin Jarjou akitajwa Azam FC pamoja na Ibrahim Imoro ambaye bado haijajulika anataka kutimkia timu gani.
Ngoma anadaiwa kusitisha mikataba wake kinyume na taratibu na hiyo kutokuwa na mwanzo mbaya ndani ya timu hiyo kutokana na kuwa na majeruhi wa mara kadhaa.
Kiungo huyo tayari yupo Dar es Salaam akisubiri barua yake ya kumalizana na Al Hilal na wakati wowote anaweza kusaini Simba tofauti na ilivyozushwa kuwa atasaini Yanga au Azam FC.
Wachezaji hao ambao wapo chini ya kocha Florent Ibenge wako njiapanda kwani hatima ya maombi yao ya kusitisha mikataba haijafika tamati.
Mchezaji Aliyesajiliwa Simba Sc ni Mauzauza
Ngoma Siyo kiwango cha simba sc, ni kama Sawadogo tu.
"Kwa kiwango cha Fabrice Ngoma na malengo ya Simba nadhani pale wamezika tu pesa zao kama ilivyokuwa kwa Sawadogo,nadhani Simba wangetafuta mchezaji mungine tu lakini Kwa Ngoma wametupa pesa zao" @alexngereza._
Mbali na hayo zipo tetesi ni kuwa Ngoma alikua hajamalizana na mabosi wake na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kufunguliwa kesi katika vyombo vinavyohusika na wachezaji.





