Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kitakachoingia kambini Agosti 21 kwaajili ya mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Uganda
Machi Ya Coastal Union 🆚 Young Africans SC
𝗡𝗘𝗫𝗧 𝗠𝗔𝗧𝗖𝗛🔰
⚽️Coastal Union 🆚 Young Africans SC
🗓 20 Agosti 2022
⏱ 10:00 Jioni
🏟 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
🏆 #LigiKuu
#TimuYaWananchi
#DaimaMbeleNyumaMwiko
Diamond Platumz Atanga Kudhamini Mashindano na Wasafibet
Mkurugenzi wa WASAFI BET Diamond Platnumz, ametangaza kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu ya Ndondo CUP kupitia Kampuni yake ya michezo ya kubashiri ya WASAFI BET.
Ndondo Cup ni bidhaa ya Clouds Media inayosimamiwa na Mchambuzi Gwiji Shaffih Dauda. #MillardAyoSPORTS.
Soka: Wachezaji 9 Wa Simba SC 9️⃣ wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars
Wachezaji wetu 9️⃣ wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars 🇹🇿 kujiandaa na michezo ya kufuzu CHAN.
▪️ Aishi Manula
▪️ Beno Kakolanya
▪️ Shomari Kapombe
▪️ Mohamed Hussein
▪️ Kennedy Juma
▪️ Jonas Mkude
▪️ Mzamiru Yassin
▪️ Kibu Denis
▪️ Habibu Kyombo
#NguvuMoja
Full Time: Yanga Sc Vs Polisi Tanzaniq
Clabu ya Yanga imeifunga timu ya Polisi Tanzania Ambapo Yanga Imeifunga Magoli Mawili Huku Polisi Tanzania Wakifunga Goli moja
Mchezo umefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
POLISI TZ 1-2 YANGA
⚽Kipemba 34'
⚽Mayele 42'
⚽Mwamnyeto 85'
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara,Yanga wameanza kampeni za kuutetea ubingwa wao kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika dimba la Sheikh Amri Abeid
Mpole, Sitofahamu Chezo wa Simba Sc Vs Geita Gold
Kuelekea mchezo wa kesho kati ya Geita Gold na Simba SC, Geita Gold ipo kwenye sintofahamu juu ya mshambuliaji George Mpole ambaye hayupo kambini na amethibitisha kuwa ana ofa kutoka nje ya Nchi anazishughulikia na mambo yakikaa sawa ataondoka.
Katika mahojiano na EFM SPORT HQ mfungaji huyo Bora wa NBCPL 2021/22 amethibitisha kuwa mkataba wake na Geita Gold umekwisha.
Source: #KitengeSports
TFF YATOA MAJINA YA WATAKAO CHEZESHA MPIRA NGAO YA JAMII
Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ngao ya Jamii 2022
@yangasc @simbasctanzania @azamsports2 @ligikuu @nbc_tanzania
Manara Avamia Kambi Ya Simba.
Afisa Muhamasishaji wa Yanga Haji Manara ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la soka nchini TFF, leo ameonekana City Lounge Hotel ambako inasemekana Simba imeweka kambi kwa ajili ya mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Haijafahamika Manara alifuata nini hapo, lakini picha za mitandaoni leo zinamuonesha Manara akiwa eneo la mapokezi la Hotel hiyo.
Source: #KitengeSports
MENEJA UWANJA WA MKAPA AONDOLEWA
TAARIFA: Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo, Agosti 9, 2022 amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi kumpangia majukumu mengine Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Bw. Godon Nsajigwa.
Taarifa iliyotolewa na Dkt. Abbasi inasema kuwa Meneja huyo anapangiwa majukumu mengine kwa kushindwa kusimamia matumizi endelevu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akieleza utekelezaji wa agizo hilo, amesema tayari taratibu zimekwishaanza za kupangiwa majukumu mengine na nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa mara moja.
Source: #KitengeSports
RAISI WA FIFA ATUA TANZANIA
Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA) Gianni Infantino ametua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kwa kuhudhuria mkutano wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) unaofanyika Arusha.
Ameongozana mwamuzi wa kimataifa mstaafu Pierluigi Collina.
YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL
YANGA YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA BRAZIL
Klabu ya Yanga imefikia makubaliano na klabu ya Singida Big Stars juu ya kubadilishana wachezaji Mbrazil Dario Federico Da'Silva JR na Jesus Moloko.
Mbrazil huyo atajiunga na Yanga SC huku Moloko akienda upande wa pili
Kila kitu kinaenda sawa mezani huku dili hilo likitarajiwa kukamilika kabla ya dirisha kufungwa Agosti 31.
#KitengeSports
𝗡𝗬𝗢𝗧𝗔 𝗪𝗔 𝗭𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝗔𝗙𝗔𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗗𝗨𝗡𝗜𝗔
𝗡𝗬𝗢𝗧𝗔 𝗪𝗔 𝗭𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝗔𝗙𝗔𝗥𝗜𝗞𝗜 𝗗𝗨𝗡𝗜𝗔
#TANZIA: Nyota wa zamani wa Simba na timu ya taifa Iddy Suleiman kibode (Meya) amefariki usiku wa kumkia leo Agosti 8, 2022 katika Hospitali ya Muhimbili. Awali Iddy alilazwa katika hospitali ya Mwananyamala na juzi usiku alihamishiwa Muhimbili.
Idd ni mdogo wa nyota wa zamani, Madaraka Seleman (Mzee wa Kiminyio).
Taratibu za mazishi kitafanyika nyumbani kwao Manzese.
*Source: KitengeSports)
CAF YATOA RATIBA YA LIGI 2022/23
CAF YATOA RATIBA YA LIGI 2022
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya timu zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu wa 2022/23 huku Tanzania 🇹🇿 ikiwakilishwa na Simba, Yanga (Ligi ya Mabingwa Afrika) na timu zote zitaanzia hatua ya awali na Kombe la Shirikisho zitakuwepo Geita Gold na Azam FC ambayo ni timu pekee 🇹🇿 itaanzia hatua inayofuata.
Droo itafanyika kesho Agosti 9 jijini Cairo, Misri.
Magazeti Ya Leo - Magazeti ya Michezo
Magazeti Ya Leo - Magazeti ya Michezo
Karibu kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania,





FULL TIME: London Stadium West Ham Utd VS Man City
FULL TIME: #EPL
🏟️ London Stadium
West Ham Utd 0-2 Man City
⚽⚽ Haaland (P) 36' 65'
Mabingwa watetezi wa ligi kuu England, Man City wameanza vyema kampeni za kutafuta ubingwa wa tatu mfululizo wa ligi hiyo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wagonga Nyundo, West Ham United.
Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic
Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili Dejan Georgijevic
Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Kimataifa wa Serbia, Dejan Georgijevic kutoka klabu ya NK Domzale.
Georgijevic (28) amesaini mkataba wa mkataba wa miaka miwili kama mapendekezo ya kocha Zoran Maki.
Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa
Simba Yauza Jezi Zote, Wengine wakosa
"🚨 Jezi zote ambazo zililetwa awamu ya kwanza zimekwisha. Mzigo mpya utakuwepo madukani ndani ya siku mbili zijazo. #SimbaNaVunjaBei #SimbaWeek #SimbaDay #SimbaDay2022 #NguvuMoja "
Wameandika Simba Katika Mtandao Wa Facebook
TETESI: MAN. UNITED YAGEUKA KWA LEROY SANE
TETESI: MAN. UNITED YAGEUKA KWA LEROY SANE
Manchester United inataka kumsajili Winga wa Bayern Munich, Leroy Sane na imeanza mazungumzo na Bayern
Sane ambaye amewahi kuichezea Man. City ana mkataba wa miaka mitatu kutumikia Bayern.
MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"
MANARA, "NIMEINGIA KAMA MC WALA SIJIHUSISHI NA MPIRA"
Aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema ameshiriki kwenye Siku ya Mwananchi kama mshereheshaji (MC) na sio kama mhamasishaji.
Manara amesema hayo baada ya kutambulisha kikosi cha Yanga mwaka 2022/2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.
Manara na Raisi wa Yanga Kukiona Cha Moto TFF.
TAARIFA: Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa ofisa wa klabu hiyo Haji Manara.
Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo.
Naye Mhandisi Said amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na Ibara ya 16(1)(a) ya Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.
Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF tayari amepelekewa mashtaka hayo, walala mikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati hiyo kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo.






































