KAONEKA: KAMA NITARUDIA PAMBANO NA MANDONGA, SITAFANYA MAZOEZI
Bondia Shabani Kaoneka aliyempiga kwa TKO Karim Mandonga amesema yupo tayari kwa pambano la marudio
> Amesema hatafanya mazoezi ili kupambana na Mandonga kwa kuwa udhaifu wake anaujua
KAONEKA: KAMA NITARUDIA PAMBANO NA MANDONGA, SITAFANYA MAZOEZI
Bondia Shabani Kaoneka aliyempiga kwa TKO Karim Mandonga amesema yupo tayari kwa pambano la marudio
> Amesema hatafanya mazoezi ili kupambana na Mandonga kwa kuwa udhaifu wake anaujua
Baada ya kuchapwa kwa Technical Knock Out, Karim Mandonga ametoboa siri ya kipigo huku akiwaomba mashabiki wake kutorudi nyuma.
"Mpinzani wangu alinipiga right (ngumi ya kulia) akaunganisha na left hook, nikayumba, wakati natambalia mikono nikitaka kunyanyuka refarii akamaliza pambano," amesema Mandonga alipokuwa akizungumza na Mwananchi Digital.
Amesema Mandonga mtu kazi yuko fiti na mashabiki wake wasirudi nyuma kwani kukosea leo sio kukosea kesho.
"Michezo yetu ni ya makosa, ukifanya kosa moja mwenzako tumia kukumaliza, ndicho kimetokea kwangu," amesema.
Mandonga amechapwa kwa TKO na Shaban Kaoneka raundi ya nne ya pambano lililopigwa mjini Songea usiku wa kuamkia leo.
"Nilijitahidi sana kupambana, lakini jitihada zangu ziliishia pale, lakini matokeo yale hayatanirudisha nyuma, sasa nataka kuzichapa na watu wenye rekodi bora kwenye ngumi, hasa wakongwe.
"Nikirudi Dar es Salaam naenda kupiga kambi na mabondia wa Ngome nikajifue jeshini hivyo atajayefuata kazi anayo," amesema.
Kuhusu tambo zake zilizomtambulisha zaidi kwenye ndondi, Mandonga amesema kila mmoja Mungu kamuandaa na kumpa kipaji chake.
"Naamini mimi kaniandaa hivi na nafsi yangu ilishakubali kupambana ," amesema bondia huyo anayepigania uzani wa super middle.
BONDIA MANDONGA APIGWA KWA KO
Bondia Karim Mandonga amepoteza dhidi ya Shabani Kaoneka, Raundi ya 4 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea
Baada ya pambano Mandonga amesema: "Ni ajali kazini lakini nipo tayari kurudiana na mpinzani wangu."