Mashabiki Walio Imba Wimbo Wa Rais wa Urusi Vladimir Putin Kuchunguzwa

 

UEFA inachunguza tukio la mashabiki wa klabu ya Fenerbahçe kuliimba jina la Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa kipigo cha 2-1 dhidi ya klabu ya Dynamo Kiev ya Ukraine wakati wa mchezo wa kufuzu Ligi ya Mabingwa.


Nyimbo hizo zilisikika katika uwanja wa Fenerbahçe mjini Istanbul muda mfupi baada ya Vitaliy Buyalskiy kuifungia  Dynamo goli la utangulizi katika mchezo ambao klabu hiyo ya Ukraine ilisonga mbele katika muda wa ziada.


"Mkaguzi wa Maadili na Nidhamu wa UEFA atafanya uchunguzi wa kinidhamu kuhusu madai ya utovu wa nidhamu wa wafuasi wa Fenerbahçe,” imesema UEFA


Klabu ya Fenerbahçe imesema ilikataza nyimbo hizo na kwamba sio haki kuilaumu klabu hiyo lakini imedai kuwa mashabiki walichokozwa na ishara za uchochezi kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa timu pinzani.


Source: #KitengeSports

No comments:

Post a Comment